Psalms 50:9-13

9 aSina haja ya fahali wa banda lako,
au mbuzi wa zizi lako.
10 bKwa maana kila mnyama wa msituni ni wangu,
na pia makundi ya mifugo juu ya vilima elfu.
11 cNinamjua kila ndege mlimani,
nao viumbe wa kondeni ni wangu.
12 dKama ningekuwa na njaa, nisingewaambia ninyi,
kwa maana ulimwengu ni wangu,
pamoja na vyote vilivyomo ndani yake.
13Je, mimi hula nyama ya mafahali
au kunywa damu ya mbuzi?
Copyright information for SwhNEN